Mazingira FM

Watu 14 wamepoteza maisha wakiwemo wanahabari watano m

January 13, 2022, 6:24 am

Watu 14 wamepoteza maisha wakiwemo wanahabari watano na abiria wa kawaida katika ajali iliyohusisha magari mawili ikiwa moja ni la abiria aina ya Toyota Hiace na jingine lenye namba za usajili STK 8140 mali ya Serikali lililokuwa limebeba waandishi wa habari mkoa wa Mwanza wakitokea Mwanza kuelekea Ukerewe kupitia Bunda, Mara kugongana uso kwa uso leo Jumanne 11, 2022.

Gari la waandishi wa habari lililokuwa kwenye msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza (RC), Robert Gabriel limegongana na gari ya abiria aina ya Toyota Hiace katika eneo la Nyamikoma wilaya ya Busega Mkoani Simiyu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Blasius Chatanda amethibitisha kutokea kwa ajari hiyo ambapo amesema chanzo Cha ajari hiyo ni mwendokasi wa magari yote mawili yaaani gari la waandishi na gari la abiria Aina ya haice

Chatanda ametoa wito kwa madereva kuzingatia Sheria za usalama Barabarani na kuepuka mwendo Kasi wakiwa wanaendesha magari maana wanakuwa wamebeba roho za watu

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Gabriel Luhumbi amesema msiba wa waandishi watano ni mkubwa na kuwa walikuwa kwenye msafara wa wa Mkuu wa Mkoa kukagua shughuli za maendeleo Wilayani ukerewe hivyo wao kama Mkoa watashiriki katika kuhakikisha Marehemu wanapewa heshima zao za mwisho

Mh Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasani ametoa Salam za rambirambi kufuatia ajari hiyo ambapo amesema

Waandishi Waliofariki ni
1.Husna Milanzi – ITV
2.Johari Shani – Uhuru Digital
3.Antony Chuwa – Freelancer
4.Abel Ngapenda – Afisa Habari ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza
5.Steven Msengi – Afisa Habari Ukerewe.

Majeruhi.
1.Tunu Heman – Freelancer
2 Vany Charles – Icon TV