Mazingira FM

TANAPA Bunda yadhamiria kuurejesha mlima balili katika asili yake.

3 December 2021, 7:11 am

Zaidi ya miche ya miti 5700 imepandwa katika eneo la safu za mlima Balili, Halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara ili kuendelea kuhifadhi na kutunza mazingira.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo lililofanyika katika eneo la Tanapa kanda ya magharibi lililopo mtaa wa Rubana kata ya Balili, Kamishina Msaidizi wa Uhifadhili na Maendeleo ya Utalii, Neema Philipo Mollel amesema wamefikia uamuzi huo ili kuurejesha mlima Balili katika hali yake

Neema philipo mollel Kamishina Msaidizi wa Uhifadhili na Maendeleo ya Utalii

Kwa upande wake Afisa Uhifadhi, Habari na Mawasiliano Tanapa Kanda ya Magharibi Bunda, Brigitha Kimario amesema katika eneo hilo linalotarajiwa kujengwa ofisi za Tanapa Kanda ya Magharibi pamefanyika uharibifu mkubwa wa mazingira kwa kukata miti kwa ajili ya mkaa na kuni ambapo zoezi hili limefanyika kwa kuwashirikisha wanafunzi ili kuwahamasisha kuwa watunzaji wa mazingira ya baadae

Brigitha Kimario Afisa Uhifadhi Habari na Mawasiliano Tanapa Kanda ya Magharibi

Naye Afisa Mtendaji Kata ya Balili, Ester Gidion amewashukuru TANAPA na TLS kwa kuendesha zoezi hilo katika kata ya Balili na kuahidi kuisimamia miche hiyo huku akitoa wito kwa jamii kuendelea kuhifadhi mazingira na atakaye kiuka atachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria

Ester Gidion Afisa Mtendaji Kata ya Balili

By Edward Lucas