Mazingira FM

Mtelela:-TAKUKURU ichunguzeni TARURA Bunda mjini

28 November 2021, 8:00 am

Salum Mtelela katibu tawala Wilaya ya Bunda akitoa maelekezo kwa TAKUKURU kuichunguza TARURA

Katibu tawala Wilaya ya Bunda Salum Mtelela ameelekeza TAKUKURU Wilaya ya Bunda kuichunguza TARURA Bunda Mjini kutokana na malalamiko mbalimbali ya utekelezaji usiyofaa wa miradi ya miundombinu ya Barabara ndani ya Halmashauri ya Mji wa Bunda

Maelekezo hayo ameyatoa kwenye kikao Cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Mji wa Bunda kilichokaa Leo Nov 22, 2021 ambapo michango ya Madiwani kwenye hoja zao wamekilaumu chombo hicho (TARURA) kushindwa kuwashirikisha Madiwani katika utengenezaji wa Barabara katika kata zao Jambo linalopelekea kulimwa kwa Barabara za kawaida na kuacha Barabara korofi

viongozi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda katika kikao Cha robo ya kwanza ya mwaka Baraza la Madiwani

Katika michango hiyo Madiwani pia wameilaumu TARURA pia kushindwa kutoa taarifa ya kiasi Cha fedha inayotolewa kwa ajiri ya kutengeneza Barabara katika kila kata

By Adelinus Banenwa