Mazingira FM

DC Nassar: Afunga shughuli za uchimbaji Madini Mgodi wa Kunanga Stooni baada ya mmoja kufukiwa na kifusi

28 November 2021, 7:35 am

DC Nassar akizungumza na wachimbaji Kunanga

Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Sharifu Mriba 26 mzanaki mkazi wa kyabakali amepoteza Maisha wakati akichimba Madini Mgodi wa Kunanga

Tukio hilo limetokea tarehe 17 Nov 2021 katika machimbo ya Kunanga Stooni kinyambwiga kata ya Guta Halmashauri ya Mji wa Bunda ambapo kwa Mujibu wa mashuhuda wamesema walipata taarifa kutoka kwa mchimbaji aliyekuwa na Marehemu ndani ya Duara ambaye yeye alinusulika baada ya Duara hilo kuporomoka ambapo baada ya kutoa taarifa alitokomea kusiko julikana kwa kuwa eneo hilo lilikuwa na zuio la kimahakama kuendelea na uchimbaji

duara lililoporomoka

Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mh Joshua Nassar amefika eneo la tukio hilo na amesimamisha shughuli zote za uchimbaji katika machimbo ya kinyambwiga kutokana na hali ya mvua zinazoendelea kunyesha jambo ambalo amesema ni hatari kwa wananchi na wachimbaji kwa ujumla lakini pia kutii zuio la kimahakama lililotolewa

By Adelinus Banenwa