Mazingira FM

Mbegu za pamba sasa wakulima kukopeshwa

12 November 2021, 5:20 pm

wakulima wa pamba kunzugu wakipokea mbegu kwenye kituo cha AMCOS baada ya utaratibu wa kukopeshwa kuanza

Siku moja tangu utaratibu wa kugawa mbegu kwa wakulima kwa njia ya mkopo kuanza kwenye AMCOS ya Kunzugu mkulima mwezeshaji na katibu wa chama hicho cha ushirika amesema mbegu zote zimeisha kwa yale makampuni yaliyoleta fomu za kujaza wakulima wanaokopa mbegu

Baada ya uongozi wa AMCOS Kata ya Kunzugu kuwatangazia wakulima utaratibu mpya wa kupata mbegu ya pamba, wengi wamejitokeza katika ofisi za AMCOS kwa ajili ya kuchukua mbegu.

Akizungumza na Radio Mazingira Fm, Katibu wa AMCOS kata ya Kunzugu Halmashauri ya mji wa Bunda, Nyang’era Lukiko amesema baada ya kupokea maelekezo mapya kutoka kwa makampuni ya kusambaza mbegu yakielekeza wakulima wakopeshwe mbegu tangia tarehe 11 November 2021 amekuwa akipokea msululu wa wakulima jambo linaloashiria mbegu zilizopo gharani zitapelea.

baadhi ya wananchi wa kunzugu wakisubili kukopeshwa mbegu za pamba baada ya utaratibu wa kununua kwa pesa tasilimu kubadirishwa

Amesema katika mifuko 330 ya mbegu alizopewa na makampuni hadi kufikia tarehe 8 November 2021 kwa utaratibu wa awali alikuwa ameuza mifuko miwili pekee kwa zaidi ya mwezi mmoja lakini tangu alipoanza utaratibu mpya wa kuwakopesha wakulima ndani ya siku mbili tu mbegu zimekwisha.

“Kwanzia leo ninavyozungumza tarehe 12 mwezi wa 11 mkopo unaendelea na wakulima wameitikia wanamiminika na mifuko leo imeisha kwa yale makampuni yaliyoleta fomu za kuwajaza wakulima wanaokopa zilizobaki ni mifuko 60 amabayo kampuni iliyoleta haijatoa fomu kwa ajili ya wakulima”

Nyang’era amesema tayari ameanza kufanya utaratibu wa kuagiza mbegu zingine kwani kituo chao kinapaswa kupokea kilo 8,000 na mpaka sasa ni kilo 6,600 tu ndizo walizopokea.

Kwa upande wao wananchi wameshukuru utaratibu huu wa kukopeshwa pembejeo na kusema baadhi walishindwa kununua mbegu hizo kutokana na ukosefu wa pesa.

By Edward