Mazingira FM

Maafali ya 1 shule ya sekondari Anthony Mtaka

10 November 2021, 8:45 pm

Wanafunzi kidato cha nne shule ya Sekondari ANTHONY MTAKA SIMIYU

Takribani wanafunzi 243 Shule ya sekondari Anthony Mtaka iliyopo Wilayani Busega Mkoani Simiyu wanatalajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu kidato cha nne  mwaka 2021 ambapo kati yao wavulana ni 104 Na wasichana ni 139

Kupitia risala ya wahitimu  kawe mgeni rasmi  katika maafali   ya wahitimu hao wameeleza kuwa pamoja na mafanikio waliyonayo Ila wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutokuwepo na bweni la wasichana, viti na meza, maktaba, Tanakirishi na walimu wa tanakirishi

Kwa upande wake makamu mkuu wa shule Mwl. Godluck Tesha akisoma risala ya shule amesema shule inajumla ya wanafunzi 1356 ambapo wavulana 674 na 682 ni wasichana huku wahitimu ni 243

Tesha ameongeza kuwa changamoto zinazoikabili shule kwa sasa ni pamoja na 1.Mabweni ya wanafunzi wanaoishi mbali na shule hasa wanafunzi wa kike, Nyumba za waalimu, Jengo la utawala Na Utoro sugu na ule wa lejaleja

Naye mgeni Rasmi ambaye pia ni mwenyekiti wa kijiji Cha Lukungu kata ya Lamadi Wilayani Busega Mkoani Simiyu mh Gerad Matias Amewataka wazazi kuwalinda wanafunzi waliohitimu kwa kuwa hatua wanayoimaliza bado wanaitaji kusonga mbele pia amewataka wazazi kuacha migogoro na walimu na punde akiwa na shida wafike shuleni kutatua changamoto hizo kwa pamoja badala ya kuleta migogoro

By Adelinus Banenwa