Mazingira FM

Wananchi wa Miembeni kata Bunda stoo wachimba Barabara kwa zana zao za asili

September 28, 2021, 4:48 pm

Wananchi wa mtaa wa Miembeni kata ya Bunda stoo Halmashauri ya Mji wa Bunda mkoani Mara, wameamua kuchonga barabara za mitaa yao kwa kutumia zana za asili baada ya kukosa huduma hiyo kwa muda mrefu.

Wakizungumza na Radio Mazingira fm katika maeneo hayo wananchi wamesema kuwa kimekuwa kilio cha muda mrefu kwa kukosa barabara za mitaa jambo linalosababisha adha kwa mama wajawazito pindi wapotaka kwenda kujifungua pamoja na wanafunzi kipindi cha mvua hawaendi shule.

Wamebaisha kuwa kwa kushirikiana na diwani wa kata hiyo wameamua kuchonga barabara hiyo ili kupunguza changamoto hiyo ikitajwa kipindi cha mvua hali inakuwa mbaya zaidi.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Bunda stoo Flavian Chacha amesema baada ya mkutano alioufanya kwenye mtaa huo wa kusikiriza kero za wananchi alibaini shida kubwa ni maji na barabara hivyo nayeye amejitolea na wananchi wake kuzifungua barabara zote ambazo hazipitiki katika kata nzima ya bunda stoo.

Ikumbukwe kwamba Mkuu wa wilaya ya Bunda Mh Joshua Nassar ameitolea wito jamii ya watu wa bunda kuwa na moyo wa kujitolea katika kuleta maendeleo kwa kuwa maendeleo yanaletwa na wananchi wenyewe.

By Adelinus Banenwa