Mazingira FM

Mbunge wa Bunda mjini Robert Mabotto Afanya Ziara kata ya Nyasura

28 September 2021, 4:26 pm

Mh Mabotto kikikabidhi baadhi ya mahitaji kwa mkuu wa gereza la Bunda

mbunge wa Jimbo la Bunda mjini Mh Robert Chacha Mabotto ametoa vifaa vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milion mbili kwenye gereza la Bunda lililoko kata ya Nyasura Halmashauri ya Mji wa Bunda

katika Ziara hiyo mh Mabotto aliongozana na viongozi wa kata hiyo pamoja na Katibu wa CCM Wilaya ya Bunda Ramadan Daro ambapo pamoja na mambo mengine alisema changamoto Zao amezibeba

magigi Samwel Kiboko Diwani wa Nyasura akipokea shilingi milion mbili kwa ajiri ya ujenzi wa boma la shule

Katika hatua nyingine Mh Mabotto alifanya mkutano wa hadhara Nyasura senta ili kusikiliza kero za wananchi ambapo pamoja na mambo mengine alichangia shilingi milion mbili kwa ajiri ya kuongeza nguvu kwa wananchi katika ujenzi wa shule ya msingi Nyasura

kwa upande wa wananchi wamebainisha kuwa kero yao kubwa ni suala la Barabara hazipitiki pamoja na gharama za bili za Maji ndani ya Mji wa Bunda.

” unit 1 ya Maji kwa Bunda ni shilingi 1862 huku kilometa 10 kutoka ziwani wakati nzega ambapo unit 1 ya Maji ni shilingi 1300 sasa hapo tumemtua mama ndio kichwa tumeweka ndoo mfukoni” alisema mwananchi mmoja.

Ramadan Daro katibu wa CCM Wilaya ya Bunda

akitoa ufafanuzi wa suala hilo katibu wa CCM Wilaya ya Bunda Ramadan Daro amesema yeye kwa kushirikiana na serikali ndani ya Wilaya ya Bunda waliwasilisha malalamiko hayo kwa waziri wa maji Jumaa Aweso na kuhaidi kwenda kulishughulikia

naye Diwani wa Kata hiyo mh Magigi Samwel Kiboko amesema tangu aingie madarakani desemba mwaka Jana ameshapokea fedha za maendeleo ndani ya kata yake zaidi ya shilingi milion miamoja na therathin hivyo amewatoa hofu viongozi na wananchi kwamba kila shilingi inayokusanywa itasimamiwa vizuri.

By Adelinus Banenwa