Mazingira FM

Aweso: aagiza matumizi bora ya maji ya mabonde ya mito

16 September 2021, 9:42 am

By Thomas Masalu

Jumaa Aweso waziri wa maji

Waziri wa maji mheshimiwa Jumaa Aweso ameagiza bodi za maji za mabonde nchini kuhakikisha wanaandaa mipango ya matumizi ya maji katika mabonde madogo ili kuhakikisha matumizi bora ya maji katika shughuli za kijamii na kiuchumi.

Aweso ametoa agizo hilo leo katika maadhimisho ya siku ya Mto Mara ambapo yamefanyika katika viwanja vya chuo cha ualimu Tarime na kwamba haya ni maadhimisho ya kumi toka yaanze kwa makubaliano ya nchi ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na serikali ya Jamhuri ya watu wa Kenya.