Mazingira FM

Thomas Masalu mtangazaji Radio Mazingira Fm mshindi wa Tuzo za umahiri EJAT 2020 nafasi ya utalii na uhifadhi

September 10, 2021, 8:09 pm

by Adelinus Banenwa

Thomas Masalu mtangazaji Radio Mazingira Fm mshindi wa Tuzo za umahiri EJAT 2020 nafasi ya utalii na uhifadhi

Mwandishi na mtangazaji wa redio mazingira fm Thomas Masalu ametwaa Tuzo ya Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT)2020  katika kipengele cha habari za Utalii na uhifadhi.

akizungumza na mazingira baada ya kutangazwa mshindi thomas amesema

Washindi wa Tuzo za Umahiri za Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT)2020 wamejulikana leo katika kilele cha sherehe za kuwapa Tuzo zilizofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mwalimu Nyerere, Jijini Dar es Salaam.

Wanahabari 59 waliteuliwa kuwania tuzo hizo za EJAT ambapo washindi wa makundi mbalimbali ya EJAT na wa jumla wametangazwa katika sherehe zilizoanza saa nane mchana hadi saa kumi na mbili jioni.

Kutokana tahadhari za janga la Covid-19, sherehe hizo za EJAT zimefanyika kwa njia ya mtandao.

Radio Mazingira Fm inakupongza kwa ushindi huo TM kaka mkubwa