Mazingira FM

Mh Mabotto: wananchi wa bunda mjini wamevumilia sana mradi wa maji

10 September 2021, 10:12 am

By Adelinus Banenwa

Mh Robert Chacha Mabotto Mbunge wa jimbo la Bunda Mjini

Mbunge wa jimbo la Bunda Mjini Mh Robert Chacha Mabotto  amewataka wananchi wa jimbo hilo kuendelea kuwa wavumilivu kwenye suala la mradi wa maji kwa kuwa bado anazidi kulipigania

Akizungumza na Radio Mazingira FM kwa njia ya simu mapema leo  kutokea Dodoma  Mh Mabotto amesema wananchi wa bunda mjini wamevumilia kwa muda mrefu kuhusu swala maji na yeye analifuatilia kwa ukaribu kuhakikisha kata zote za Bunda mjini zinapata maji

Ikumbukwe kwamba Mh Mabotto yuko Bungeni Jijini Dodoma kuhudhuria vikao vya Bunge ambapo hapo jana aliuliza swali bungeni akitaka kujua kuhusu mradi wa maji wa Bunda mjini wenye thamani ya bilioni 10.6 hadi sasa zimeishatolewa billion 2.6 tu ikiwa bado billion 8 je serikali itamalizia lini fedha hizo ili mradi uweze kukamilika.