Mazingira FM

Mtangazaji wa Mazingira Fm Thomas Masalu amefanikiwa kutinga fainali za tuzo za umahiri (EJAT) 2020.

September 2, 2021, 8:17 am

Tuzo hizo zinazoandaliwa na baraza la habari Tanzania MCT, ndiyo tuzo kubwa zaidi za uandishi wa habari nchini, zinazopimwa kwa kushindanisha kazi Bora zilizowahi kuripotiwa nchini katika kipindi cha mwaka mzima.

thomas masalu

Thomas Masalu Mtangazaji na mwandishi wa Habari kutoka radio Mazingira fm iliyopo Bunda mkoani Mara ndiye mwandishi pekee aliyeingia kwenye fainali hizo akiwakirisha mkoa wa Mara

Kati ya jumla ya kazi Bora za habari 59 zilizotangazwa na MCT kuingia katika fainali hizo baada ya mchujo, Redio Mazingira fm imefanikiwa kuchomoza katika fainali hizo.