Mazingira FM

Aliyekuwa DC Bunda aagwa baada ya kustaafu

2 September 2021, 8:56 am

By Adelinus Banenwa

Umoja wa watumishi Makada wilaya ya Bunda mkoani Mara,leo umefanya sherehe ya kumuaga aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Bunda mwalimu Lydia Bupilipili na kumkaribisha mkuu wa wilaya ya Bunda Mheshimiwa Joshua Nasarr.

Mwl, Lydia Bupilipili aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Bunda

Akizungumza wakati wa kufungua sherehe hiyo mwenyekiti wa umoja huo,Michael Nkoba amesema kuwa leo ni siku muhimu kwa umoja huo kuweka historia mpya.

Naye aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Bunda Mwalimu Lydia Bupilipili ambaye pia ndiye alikuwa anafanyiwa sherehe ya kuagwa,ametoa pongezi kwa mkuu wa wilaya ya Bunda Joshua NasarrĀ  kwamba ameanza vizuri kuchapa kazi ndani ya wilaya ya Bunda.

Hata hivyo Mkuu wa wilaya ya Bunda mheshimiwa Joshua Nasarr amesema umoja wa watumishi Makada wilaya ya Bunda umefanya jambo la mfano na kwamba Bupilipili anaweza akawa mkuu wa wilaya mstaafu wa kwanza aliyefanyiwa sherehe ya kuagwa.