Mazingira FM

Baraza la umoja wa Vijana UVCCM Wilaya ya Bunda

3 July 2021, 3:33 pm

By Adelinus Banenwa

Wambula Peresia Katibu wa UVCCM Mkoa wa Mara

Katibu wa Umoja wa Vijana UVCCM mkoa wa Mara Wambula Peresia amesema niwajibu wa madiwani na wabunge kuwawezesha Vijana hasa kwenye kuandaa mabaraza ya Wilaya

Hayo ameyasema leo July 3, 2021 kwenye baraza la Vijana UVCCM Wilaya ya Bunda ambapo amesema wajumbe wa baraza hilo kushindwa kuudhuria Baraza inatokana na kukosa uwezeshwaji.

Kupitia Baraza hilo Wambula amesema Madiwani na wabunge ni wajibu wao kutoka kila kata husika kuwawezesha Vijana kufika kuudhuria Baraza hilo

Pia Wambula amewataka Vijana kuzungumzia mazuri anayoyafanya Rais wa TANZANIA. Mh Samia Suluhu Hasani maana wapo watu wengi wanabeza Kazi anazizifanya Rais Samia

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana UVCCM Wilaya ya Bunda Gasper Petro Charles amesema kuna changamoto zinazokumba umoja huo ikiwemo kukosa miradi ya uendeshaji katika utekelezaji wa majukumu yake

Gasper Petro Charles Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Bunda

Sambamba na hilo Gasper amewakumbusha Vijana kuzingatia maadili ya chama ikiwemo kutekeleza maelekezo yote yanayotolewa na viongozi.

Wajumbe wa baraza la Vijana UVCCM Wilaya ya Bunda

Kwa upande wa Vijana ambao ni wajumbe wa baraza hilo wamesema ukweli ndiyo nguzo ya jumuhiya hiyo hivyo wamemuomba Katibu wa UVCCM Mkoa wa Mara kuwasaidia wapate ufumbuzi wa mgogoro wa kiwanja Chao ambapo wanaitaji kujenga Nyumba Katibu wa Umoja huo