Mazingira FM

Mh Nassar: Akabidhiwa ofisi na Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Bunda Mwl Lydia Bupilipili

22 June 2021, 6:39 am

By Adelinus Banenwa

makabidhiano ya ofisi ya Wilaya ya Bunda Kati ya Mh Joshua Nassar na Mwl Lydia Bupilipili

Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mh Joshua Nassar Leo June 21, 2021 amekabidhiwa ofisi na Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Bunda Mwl Lydia Bupilipili ambaye amestaafu

Mkuu wa Wilaya ya Bunda mstaafu Mwl Lydia Bupilipili akisoma taarifa ya makabidhiano
Akizungumza katika makabidhiano hayo Mh Nassar Amewataka wanabunda wote kuwa wamoja na kwa kuwa yeye ni kijana anaamini Kazi zote zitaenda kwa haraka maana damu yake bado inachemka
Katika hatua nyingine Mh Nassar amesisitiza kuwa wasimuogope maana yeye atakuwa DC anaye fikika na kila mmoja na ameahidi kufanya Kazi na vyombo vya Habari.
Mkuu mpya wa Wilayan Mh Joshua Nassar na Mkuu wa Wilaya mstaafu Mwl Lydia Bupilipili wakisaini taarifa ya makabidhiano

Naye Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Bunda Mwl Lydia Bupilipili amewashukuru wananchi wote wa Wilaya ya Bunda kwa ushirikiano waliomuonesha kwa kipindi chote akiwa mkuu wa Wilaya ya Bunda na amewasihi kumpa ushirikiano mkuu mpya wa Wilaya ya Bunda ambaye amekabidhiwa ofisi Mh Joshua Nassar