Mazingira FM

Diwani Flaviani Nyamigeko tuziunge mkono timu za nyumbani

7 June 2021, 6:15 pm

Diwani wa kata ya bunda stoo Flavian Chacha Nyamigeko amewataka wadau mbalimbali wilayani Bunda na viunga vyake kuziunga mkono timu za nyumbani ili ziweze kufanya vizuri kwenye mashindano ya kitaifa

Diwani wa Kata ya Bunda stoo Flaviani Chacha akikabidhi mahitaji ya kambi ya kwa Timu ya Bunda Queens

Hayo ameyasema leo alipotembelea kambi ya timu ya Bunda Queens inayoshiriki mpira wa miguu wa wanawake daraja la kwanza ambayo ndiyo timu pekee inayowakirisha mkoa wa Mara ambapo kambi yao ipo shule ya msingi miembeni mjini Bunda

Pichani ni Diwani wa Kata ya Bunda store Flaviani Chacha na Timu ya Bunda Queens

Diwani huyo ametoa kilo 40 za mchele, mfuko wa sabuni ya kufulia pamoja na Chumvi dazeni moja

Kwa upande wake kapteni wa timu hiyo amesema wao wamejiandaa kuiwakilisha vyema jamii ya mkoa wa Mara ila wanaitaji uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa wadau maana bado changamoto ni nyingi ikiwemo vifaa vya michezo kama mipira jezi na chakula

Naye Mwenyekiti wa timu hiyo ndugu amesema anashukuru kwa mchango wa diwani alioutoa kwa timu yake kwa kuwa Bunda Queens ni mali ya wanabunda hivyo waiunge mkono ili ikafanye vizuri kwenye mashindano ya michezo ya mpira wa miguu wa wanawake daraja la Kwanza