Mazingira FM

Bunda tayari kuupokea Mwenge wa uhuru

June 5, 2021, 3:06 pm

Mkuu wa mkoa wa Mara Mh Mhandisi Gabriel Luhumbi amekagua miradi ambapo Mwenge wa uhuru utapita kuizindua ndani ya Wilaya ya Bunda

Mkuu wa mkoa wa Mara Mhandisi Gabriel Luhumbi akikagua sehemu Mwenge wa uhuru utakapolala Wilayani Bunda

Miradi iliyokaguliwa ni pamoja na kituo Cha Afya Cha Nyamuswa (IKIZU), mradi wa Maji wa kihumbu Hunyari, mradi wa matrekta ya AMCOS kunzugu, Taa za Barabarani mjini Bunda, Zahanati ya RC Bunda stoo, kiwanda Cha Tofari kinachomilikiwa na Halmashauri ya Mji wa Bunda

Mh Luhumbi katika ziara hiyo ndani ya Wilaya ya Bunda alikuwa na mwenyeji wake Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mh Mwl Lydia Bupilipili pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ambapo DC Bupilipili amesema Wilaya ya Bunda imejipanga kuupokea Mwenge wa uhuru huku akibainisha shughuri zitakazofanyika ni pamoja na Upimaji wa VVU kwa hiali, masuala ya chakula na Lishe kwa akina mama, watoto, wamama wajawazito pamoja na wazee

Mwenge wa uhuru unatarajiwa kufika Wilaya ya Bunda June 27, 2021 ukitokea wilaya ya Butiama na kukabidhiwa wilaya ya Busega mkoani Simiyu tarehe 28 June 2021