Mazingira FM

Dkt Tinuga; Serikali inatambua mchango mkubwa wa wauguzi

May 24, 2021, 11:59 am

Maadhimisho ya siku ya wauguzi Duniani kwa mkoa wa Mara imefanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda ambapo mgeni Rasmi alikuwa mganga mkuu wa mkoa wa Mara DKT FROLIAN TINUGA  kwa niaba ya katibu tawala wa mkoa

FROLIAN TINUGA Mganga mkuu wa mkoa wa Mara
Wauguzi wakiwa kwenye maandamano kuadhimisha siku ya wauguzi Duniani
wauguzi wakitoa msaada kwa wagonjwa siku ya wauguzi Duniani

Katika kujibu risala ya wauguzi Dkt Tinuga amewakumbusha baadhi ya  wauguzi kuhakikisha wanafanyia kazi changamoto ambazo mara nyingi wagonjwa huwalalamikia pale wanapopata huduma licha ya kwamba Wauguzi hao wanatoa mchango mkubwa sana katika idara ya Afya

Awali mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda mwl Amosi Kusaja aliwapongeza wauguzi kwa kuwa mstari wa mbele katika kutetea maisha ya watu licha ya changamoto nyingi wanazokabiliana nazo

Naye mkuu wa wilaya ya Bunda kama mgeni wa heshima katika maadhimisho hayo amesema anatambua mchango wa wauguzi hasa kwa kutokuwa wabaguzi kwa wagonjwa pasipokujali hali ya mgonjwa tofauti na fani zingine

Awali akisoma risala mwenyekiti wa wauguzi Mkoa wa Mara  Ngeleja Lupeleleja amesema Wauguzi wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo kutopandishwa vyeo, mishahara pamoja na idadi ndogo ya wauguzi ikilinganisha na mahitaji jambo linalopelekea wauguzi  kuhudumia wagonjwa wengi zaidi kuliko inavyoshauriwa.