Mazingira FM

Wanyamapori waaribifu waendelea kuwatesa wananchi BUNDA

May 18, 2021, 6:03 pm

Wananchi wa migungani kata ya Bunda Stoo wilaya ya Bunda mkoani Mara wamelalamikia suala la wanyama pori waaribifu ikiwemo Tembo na Viboko kuwakatisha tamaa ya kujihusisha na kilimo

Wananchi wa Bunda Stoo katika kikao na Diwani Flaviani Chacha kuhusu wanyama waaribifu

Wakizungumza katika kikao cha diwani wa kata hiyo Flaviani chacha kilicholenga kusikiliza kero za wananchi wa Butakale na Migungani wananchi hao walibainisha changamoto ya Tembo na Viboko kuwa tishio la usalama wao na mazao yao

Naye diwani wa kata hiyo Flavian Chacha amewatoa hofu wananchi na kusema kuwa kero zote walizozisema amezichukua na atazifikisha serikalini ili ziweze kutatuliwa