Mazingira FM

Milion 80 kujenga madarasa manne kata ya Bunda stoo

April 27, 2021, 6:05 am

Diwani wa kata ya bunda stoo Flaviani Chacha  amewapongeza wadau wa maendeleo kwa kuendelea kujitolea katika kuisaidia serikali kutatua kero za wananchi

Akizungumza na Redio Mazingira Fm April ,22/ 2021 Flavian amesema amepokea shilingi milion 80 kutoka kwa wadau wa maendeleo kwa ajili ya ujenzi wa madarasa manne katika shule mbili zilizopo kata ya Bunda stoo

Katika hatua nyingine ameipongeza serikali kupitia wizara ya tamisemi kuhusu madiwani kuijadili TARURA kwa maana imekuwa changamoto sana hasa katika kushughurikia barabara  za ndani

Vilevile amezungumzia upande wa nyongeza ya posho kwa madiwani Flavian amesema serikali ni lazima ilitazame kwa kuwa inaweza kuchangia madiwani kushindwa kutoa hoja kwa mkurugenzi