Mazingira FM

Kiboko; Wanaotumia TASAF kulewa kukiona

20 April 2021, 11:31 am

Diwani wa kata ya Nyasura Magigi Samwel Kiboko amewataka wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya masikini yaani TASAF kutumia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa.

akizungumza na Mazingira kwenye ofisi ya mtendaji kata ya Nyasura Kiboko amesema kwa upande wa wale wenye sifa lakini hawako kwenye mpango basi atafuatilia.

Kwa upande wake Peter Alphonce mjumbe serikali ya mtaa wa Nyasura ā€˜Dā€™ amebainisha kuwa fedha zinazotolewa na TASAF zimewasaidia kwa kiasi kikubwa wananchi wenye maisha ya hali ya chini.