Mazingira FM

Charles; Marufuku watoto kufanya biashara kwenye masoko Mara

20 April 2021, 12:26 pm

Mwenyekiti wa wajasiliamali mkoa wa Mara ndugu Charles Waitara amewataka wajasiliamali  wote mkoa wa Mara kutojihusisha na kuwaajiri watoto katika maeneo ya biashara

Charles Waitara mwenyekiti wa wajasiliamali Mkoa wa Mara

Kauli hiyo ameitoa April 19 2021  katika mkutano wa hadhara na wajasiliamali eneo la balili kona,  lakini pia amewaasa wafanyabiashara kuzingatia usafi

Naye Diwani wa kata ya Balili Thomasi Tamka amewataka wananchi wa kata ya Balili na viunga vyake vyote kuzingatia usafi wa maeneo yao ya biashara sambamba na ujenzi wa vyoo bora