Mazingira FM

Mh Waitara. Amtaka mkandarasi kufanya kazi usiku na mchana

17 April 2021, 5:26 pm

MARA: APRILI 17, 2021

NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara, amemtaka mkandarasi wa kampuni ya M/S Beijing Construction Engineering Group Company Limited, kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha kwa wakati mradi wa upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Musoma.

 

Naibu waziri wa ujenzi na uchukuzi Mh Mwita Waitara katikati

Mradi huo utagharimu zaidi ya Tsh. bilioni 30 unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 20 utahusisha barabara ya kuruka na kutua ndege, barabara ya maegesho ya ndege na jengo la zima moto. 

Akizungumza baada ya kukagua kiwanja hicho mkoani Mara, Waitara amesema kukamilika kwa kiwanja hicho kutapandisha uchumi wa mkoa na kukuza utalii katika ukanda huo.