Mazingira FM

Dc Bupilipili ; awapongeza wakulima wa pamba

April 16, 2021, 7:25 pm

 Mkuu wa wilaya ya Bunda Mwl Lydia Bupilipili amewapongeza wakulima wa zao la Pamba wilaya ya Bunda mkoani Mara  kwa kuzingatia kilimo bora na chenye tija.

Dc Bupilipili ametoa pongezi hizo leo tarehe 15 mwezi wa 4 alipofanya ziara ya kukagua mashamba ya wakulima katika maeneo ya Butakare, Buzimbwe na shule ya msingi Sazizira ili kujionea wakulima hao wanavyo lima kilimo cha zao la pamba kwa kuzingatia taratibu za kilimo.

Aidha Bupilipili amesema ili kuhakikisha wanakabiliana na mabadiliko ya tabia nchi hasa ukame wanatafuta uwezekeno wa kuboresha teknolojia ya kilimo cha umwagiliaji

Sambamba na hilo Bupilipili amewapongeza bodi ya pamba kwa kusambaza  viwatilifu kwa wakulima kwa wakati huku akivitaka vyama vya msingi  vya ushirika  kuhakikisha wanahudumia wakulima ipasavyo.