Mazingira FM

Dc Bunda: fanyeni usafi msisubiri mashindano

April 15, 2021, 10:35 am

Mheshimiwa Mkuu wa wilaya ya Bunda Mwal Lydia Bupilipili amewataka wananchi kuendelea kujenga tabia ya kufanya usafi katika maeneo yao na siyo mpaka wasubiri kusukumwa ama kusubili mashindano.

Dc Bunda Mh Mwl Lydia Bupilipili

Rai hiyo ameitoa leo wakati akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake ambapo  amesema suala la usafi linatakiwa liwepo na lifanyike muda wote huku akitoa mfano katika masoko na magengena.