Mazingira FM

Dc Bunda awapongeza wananchi kwa ushirikiano kipindi cha maombolezo

8 April 2021, 12:49 pm

Mheshimiwa mkuu wa wilaya ya Bunda mkoani Mara Mwalimu Lydia Bupilipili amewashukuru Wananchi wa wilaya Bunda kwa kuonesha mshikamano na uzalendo wakati wa kipindi chote cha maombolezo ya msiba wa  aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

Mh Lyidia Bupilipili mkuu wa wilaya ya Bunda

Bupilipili ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake.