Manyara FM

Madiwani Babati watakiwa kusimamia vyakula shuleni

9 February 2024, 5:40 pm

Picha ya pamoja na baraza la madiwani wa halimashauri ya mji wa Babati

Mwenyekiti wa Halimashauri ya mji wa Babati Abdrahaman Kololi awahimiza madiwani kusimamia chakula mashuleni katika kipindi hiki cha  mavuno.

Na Mzidalfa Zaid

Mwenyekiti wa halimashauri ya mji wa Babati Abdrahaman Kololi amewaagizi madiwani wa halimashauri hiyo kuhakikisha wanawahimiza wananchi kupeleka vyakula mashuleni katika kipindi hiki ambacho wanaendelea kuvuna mazao.

Ametoa maagizo hayo leo katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa halimashauri ya mji wa Babati, amesema kuanzia sasa wakulima wengi wanaendelea kuvuna mazao hivyo ni wajibu wa kila mzazi kuhakikisha anapeleka chakula shuleni ili mtoto asome kwa bidii.

sauti ya mwenyekiti wa halimashauri

Nae katibu wa chama cha mapinduzi ccm halimashauri ya mji wa Babati Mohamed Cholage , amewataka wazazi kuzingatia michango ya vyakula mashuleni kwakuwa itasaidia kukuza taaluma katika halimashauri.

sauti ya katibu ccm babati mji

Nao baadhi ya madiwani walioshiriki kikao hicho, wamesema agizo lililotolewa na mwenyekiti wa halimashauri watalifanyia kazi kwa kuitishavikao mbali mbali na kutoa elimu kwa wazazikuhusu umuhimu wa kupeleka chakula mashuleni.

sauti ya madiwani

Kwa upande wake mkuu wa idara ya kilimo halimashauri ya mji wa Babati Daniel Lutha, amesema hali ya uzalishaji wa chakula kwa mwaka huu ni mzuri kutokana na mvua kubwa zilizonyesha katika maeneo mbalimbali nchini.

sauti ya mkuu wa idara ya kilimo halimashauri ya mji wa babati