Manyara FM

Mlemavu wa miaka 19 abakwa Manyara

9 February 2024, 5:18 pm

picha ya kamanda wa jeshi la polisi Manyara

Jeshi la polisi mkoani Manyara linamshikilia Ramadhani Idd mwenye umri wa miaka 19 kwa kumbaka binti mwenye umri wa miaka 19 mlemavu.

Na Mzidalfa Zaid

Jeshi la polisi mkoani Manyara linamshikilia Ramadhani Idd mwenye umri wa miaka 19 kwa kosa la kumbaka binti mwenye umri wa miaka 19 ambae ni mlemavu wa kutokuongea na kusikia katika kata ya Magugu Wilayani Babati mkoani Manyara.

Taarifa hiyo imetolewa  na Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Manyara George Katabazi alipokuwa akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake,amesema ni mara ya pili binti huyo anabakwa ambapo mtuhumiwa wa kwanza alifungwa miaka 30 jela na mtuhumiwa wa pili ambae amefanya kosa hilo atachukuliwa hatua zakisheria ikiwemo kufikishwa mahakamani.

Kamanda Katabazi amesema tukio hilo limetokea february 6 mwaka huu  baada ya jeshi la polisi kupata taarifa hizo walifanya msako na kumkamata kijana huyo ambae alikuwa akijaribu kutoroka.

Sauti ya kamanda wa jeshi la polisi Manyara

Aidha,ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Manyara kutoa taarifa kwa jeshi la polisi wanapobaini vitendo vyovyote vyenye kuashiria uharifu katika maeneo yao.