Kitulo FM

mbunge Festo Sanga akabidhi fedha shule ya msingi unenemwa

September 12, 2023, 12:22 pm

MBUNGE wa jimbo la makete mh festo sanga akishiriki ujenzi wa darasa.picha na Emmanueli sanga

kutokana na uchakavu wa madarasa katika shule ya msingi unenamwa ilioko kata ya luwumbu mbunge wa jimbo la makete Mh Festo Sanga amekabidhi shilingi laki 5 na elfu sabii.

na Lulu Samson

MBUNGE wa jimbo la makete mh festo sanga amekabidhi shilingi laki 5 na elfu sabii kwa uongozi wa shule ya msingi unenamwa kukarabati madarasa ya shule hiyo
Mh sanga amekabidhi fedha hizo ambazo zitasaidia kwenye ukarabati wa madarasa ambayo wadau wa kijiji cha unenamwa na usililo kata ya luwumbu wameanza kufanya ukarabati wa madaraa hayo ambayo yamechakaa
Wannachi wa kijiji cha unenamwa wamemshukuru mh mbunge kwa kusaidia ukarabati wa madarasa hayo kwa kuunga mkono jitihada za wadau wa maendeleo kata ya luwumbu