Wadau walipowatembelea wafungwa Gereza Wilaya Ndulamo
Kitulo FM

Wanawake na Wanaume Makete wawatembelea Wafungwa Gerezani

March 7, 2023, 9:52 pm

Kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani wanawake kwa kushirikiana na wanaume Kata ya Iwawa, wametembelea wafungwa katika gereza la Wilaya ya Makete lililopo kijiji cha Ndulamo  wakiwa na lengo  la kuungana nao katika maadhimisho hayo  kwa kuwafariji na kuwapa baadhi ya mahitaji ya Msingi

Jaquline Mroso ni Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Makete amesema wameenda kuwaona wafungwa kwani ni kundi ambalo jamii linawachukulia kuwa ni wahalifu hivyo wanahitaji upendo na kuwakumbuka kwenye mahitaji na akiwaasa wafungwa hao kuona kama hapo ni mafunzoni na wakirudi uraiani wabadilike huku akiiasa jamii kufanya matendo ya huruma

Mrosso ameongeza kuwa  siku ya wanawake iwe chachu kwa jamii  kuweka utaratibu wa kuwatembelea na kuwapelekea baadhi ya mahitaji yao ya muhimu huku akimshukuru Mkurungenzi Mtendaji Wilaya ya Makete Ndg Wiliam Makufwe kwa kufanikisha kwenda kuwaona wafungwa hao na kuwapongeza  wanaume wote ambao wamejitoa kwa hali na mali kwa kutoa michango yao 

Akizungumza kwa niaba ya wanaume ambayo wameshirikiana na wanawake katika kufanikisha tukio la kuwaona wafungwa Henry Nyigu  amewapongeza wanaume kwa kuwaunga mkono wanawake kwa kutoa michango na amewaomba wanaume kushiriki katika kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani  ili kuwatia moyo na kusikiliza jumbe mbalimbali  ambazo zimeandaliwa kwa ajili ya kutoa elimu , hamasa na kuleta mabadiliko kwenye jamii

Lucy Malenya ni Afisa Tawala wa Gereza la Wilaya ya Makete amewashukuru wanawake kwa kuwatembelea na amewaomba kuendelea kuwatembea wafungwa  kwa wakati mwingine

Wanawake hao wamepeleka mahitaji mbalimbali ikiwemo sabuni za kuogea na kufulia , mafuta ya kupaka, miswaki  ,sabuni na taulo za kike mahitaji hayo yanajumla ya shilingi laki tatu miamoja sabini na tatu 

Wadau walipowatembelea wafungwa Gereza Wilaya Ndulamo
Wadau walipowatembelea wafungwa Gereza Wilaya Ndulamo