Baadhi ya Askari Polisi Wanawake wakiwa na vitu kadhaa kama zawadi kwa watoto Kituo cha Kulelea watoto Yatima Bulongwa
Kitulo FM

Polisi Wanawake Makete wawafariji Yatima Bulongwa

March 7, 2023, 9:59 pm

Mtandao wa Jeshi la Polisi Wanawake Wilayani Makete Mkoani Njombe wametembelea kituo cha kulelea watoto Yatima Bulongwa na kutoa msaada wa vitu mbali mbali vyenye thamani ya shilingi laki tatu .

Philipina mkumbo  ni Mkuu wa upelelezi Wilaya ya Makete amesema moja ya kazi kubwa wanayofanya  wanawake ndani ya Jeshi la Polisi Tanzania ni kusaidia watoto na kuwaona watoto wenye mazingira magumu pamoja na kutoa elimu kwa watoto na hata  jamii nzima namna ya kuzuia uhalifu katika maeneo yao

Kwa upande wake Mkuu wa Kituo  cha kulelea Watoto Bulongwa Vaileth Chaula amewashukuru mtandao wa Jeshi la Polisi Wanawake Makete kwa kujitoa kwao na kuwatembelea katika kituo hicho

Nao baadhi ya Askari wanawake waliohudhuria katika kituo hicho wamewapongeza walezi wa watoto hao kwa jitihada zao wanazozifanya kuhakikisha watoto wanapata malezi bora

Ikumbukwe kuwa kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani hufanyika kila tarehe nane machi ya kila mwaka ambapo kwa mwaka huu maadhimisho hayo yanakwenda sambamba na kauli mbiu isemayo  UBUNIFU NA MABADILIKO YA TEKNOLOJIA, CHACHU KATIKA KULETA USAWA WA KIJINSIA