Afisa Lishe Jackilne Nanauka akizungumza na wanafunzi wa Iwawa Sekondari walipo katika Club ya Lishe
Kitulo FM

Wanafunzi Iwawa Sekondari wapigwa Msasa kuhusu Lishe

March 6, 2023, 5:32 pm

Wanafunzi wa Iwawa Sekondari kupitia Club ya Lishe wameendelea kupata Elimu kutoka kwa wataalamu wa Afya kuhusu Lishe na vyakula bora.

Afisa Lishe Wilaya Bi. Jackline Nanauka leo Machi 6, 2023 akiwafundisha wanafunzi hao kuhusu Lishe shuleni hapo amesema Lishe ni muhimu kwa mtu yeyote hivyo wanapaswa kuhakikisha wanazingatia maelekezo wanayopewa na wataalamu na kuyatumia kikamilifu wanapokuwa nyumbani.

Nanauka amewaeleza umuhimu wa kuzingatia Lishe kwa wanafunzi, wazazi na wadogo zao wawapo nyumbani na hata katika mazingira ya shule wakati wote ili kuwa na Afya njema

Kwa upande wao wanafunzi hao wamesema elimu ya Lishe itawasaidia katika Familia zao na wataendelea kukumbushana umuhimu wa Lishe kwa Jamii ili waweze kuwa na Afya njema na kuepukana na Udumavu.