Trekta likiwa shambani wakati wa maandalizi ya Mashamba ya Ngano Kijiji cha Mbalatse
Kitulo FM

Maandalizi ya Kilimo cha Ngano yaanza Makete

March 6, 2023, 6:39 pm

Uandaaji wa Mashamba ya Ngano Kitongoji cha Ludodolelo Kijiji cha Mbalatse Wilaya ya Makete ambapo Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Makete William Makufwe akiwa na Afisa Kilimo Wilaya Aniseti Ndunguru wamefika kwenye Mashamba ya Ngano yaliyoanza kulimwa kwa Trekta eneo la Ludodolelo

Serikali imeshatoa Tani 80 za Mbegu ya ngano kwa ajili ya kugawa kwa Wakulima Wilayani Makete

Wakiwa kwenye Mashamba hayo, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Makete William Makufwe amewapongeza wataalamu wake kwa kazi nzuri na kasi inayoendelea ya kuandaa mashamba hayo ya Ngano kwenye Kitongoji cha Ludodolelo.

Afisa Kilimo Wilaya Aniseti Ndunguru amesema zaidi ya ekari 100 zimeshalimwa ambazo zinamilikiwa na wakulima mbalimbali kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Makete na wanaendelea na kilimo hivyo wanatarajia kufika tarehe 20 Machi 2023 kazi ya kulima na kupanda itakuwa tayari imeshapandwa.