Wanafunzi wahitimu wakiimba Wimbo wa kuwaga wanafunzi wenzao wanabaki kuendelea na Masomo
Kitulo FM

Wanafunzi Mwakavuta Sekondari wahimizwa kuishi katika Mungu

March 4, 2023, 7:55 pm

Wanafunzi wa Umoja wa Kikristo Tanzania (UKWATA) Shule ya Sekondari Mwakavuta leo Machi 04 wamefanya mahafali ya kuhitimi Kidato cha sita huku wakitakiwa kuendelea kuiishi Imani yao Kikamilifu katika maisha yao yote.

Wakisoma Risala yao mbele ya Mgeni Rasmi Katika Mahafali hayo Ndugu Mwamepo Sanga, wamemweleza mafanikio makubwa katika kipindi cha miaka miwili kuanzia 2021 mpaka sasa 2023 wanapohitimu masomo yao Kidato cha 6 na kusema kwamba wamekuwa wakiimarika katika utumishi kwa kuwarejesha baadhi yao waliokuwa nje ya utaratibu wa UKWATA Shuleni hapo

Mwalimu Mlezi wa UKWATA Shule ya Sekondari Mwakavuta amesema David Mgaya amesema wahitimu 40 wamehitimu mafunzo mbalimbali ya UKWATA na wamekuwa wakifanya vizuri katika mitihani yao ya Dini huku akiwaombea kwa Mwenyezi Mungu kufanikiwa vizuri zaidi katika mitihani yao ya kuhitimu Kidato cha sita watakayofanya mwezi wa 5 mwaka huu 2023.

Mgeni Rasmi katika mahafali hayo ya Ukwata Ndg. Mwamepo Sanga amewataka wanafunzi hao kuendelea kukua katika maadili yaliyo mema katika Jamii mara baada ya kuhitimu masomo yao ya Kidato cha sita

Hata hivyo katika Raisala ya wanafunzi hao wameomba mchango wa kusaidiwa kurekodi Nyimbo 3 kwa njia ya Video ambapo Mgeni rasmi ametoa kiasi cha shilingi Laki tano kusaidia uinjilishaji unaofanywa na wanafunzi hao wa UKWATA Mwakavuta Sekondari