Mtaalamu wa Afya na Mazingira akitoa maelezo namna ya kutumia choo cha Kisasa
Kitulo FM

Wahimizwa Matumizi Bora ya Vyoo Makete

March 4, 2023, 8:31 pm

Wananchi Wilayani Makete wamehimizwa matumizi bora ya vyoo vya Kisasa na kuachana na byoo vya shimo ambavyo vimepitwa na wakati.

Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ivalalila Kata ya Iwawa Mtaalamu wa Afya na Mazingira kutoka Idara ya Afya Bw. Sanga amesema matumizi ya Sink la Plastiki ambalo ni rahisi pia hata bei yake yanaweza kusaidia wananchi kuepuka magonjwa ya kuambukiza kupitia kinyesi.

Sanga amesema wananchi wanapaswa kuachana na vyoo vya shimo maarufu kama vyoo vya kulenga na kujenga vyoo vya kisasa kwa gharama nafuu ili kuwa na Jamii ya Kisasa iliyoelimika