Picha ya Mtaalamu wa Afya
Kitulo FM

Elimu ya Afya na Lishe yatolewa kwa Wanawake

March 3, 2023, 2:42 pm

Idara ya Afya Wilaya ya Makete Kitengo cha Lishe imeendelea kutoa Elimu ya Afya na Lishe kwa wanawake vijiji Mbalimbali Wilayani Makete.

Elimu hiyo ni kuhusu Lishe bora kwa watoto kuanzia miezi 6 na kuhakikisha wananyonyesha Maziwa halisi ya Mama kwa mtoto aliyechini ya Miezi 6.

Jackline Nanauka Afisa Lishe Wilaya ya Makete akiwa kijiji cha Ivalalila amezungumza na wanawake wenye watoto walipohudhuria mafunzo hayo yenye lengo la kutoa elimu ya Afya na Lishe amewasihi kuzingatia maelekezi yanayotolewa na wataalamu mara kwa mara

Elimu kuhusu Afya na Lishe imetolewa kwa wananchi hususani wanawake wenye watoto chini ya miaka 5
Afisa Lishe Wilaya ya Makete Bi. Jackline Nanauka kulia akiwa kwenye zoezi la upimaji wa urefu kwa Umri kwa watoto waliochini ya miaka mitano Kijiji cha Ivalalila