Kitulo FM

Elimu kuhusu Mikopo yatolewa kwa wananchi wa Tarafa ya Ikuwo

March 2, 2023, 12:48 pm

afisa maendeleo ya jamii akizungumza na wananchi

Maafisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Makete wameendelea na zoezi la kutoa Elimu ya Mikopo kwa Wananchi Kata mbalimbali za Wilaya ya Makete Mkoa wa Njombe.

Elimu ya mikopo hiyo ni kuhusu Maandalizi kuelekea utoaji wa Mikopo ambayo itatolewa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii na Wizara ya Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu ambapo mikopo hiyo itahusisha Wanawake na Vijana kwa masharti tofautitofauti ukiachilia mbali mikopo ya Halmashauri ya 10% amabayo itaendelea kutolewa kwa makundi ya Wanawake, Vijana na watu wenye Ulemavu kupitia Vikundi ilihali Mikopo ya Wizara anaweza kukopeshwa mtu mmoja mmoja, Kikundi, Kampuni n.k