Kitulo FM

Vifaa vya Huduma ya Dharura vimeunganishwa Hospitali ya Wilaya Makete

January 29, 2023, 8:02 am

Zoezi la kufunga vifaa tiba vya kisasa jengo la dharura (EMD) Hospital ya Wilaya ya Makete Mkoa wa Njombe limefanywa na wataalamu kwa lengo la kuanza kutoa huduma za Afya Hospitalini hapo.

Serikali imetoa Milioni 300 kujenga jengo hilo la Dharura kwa lengo la kuongeza ubora wa upatikanaji wa huduma za Afya kwa wagonjwa wa Dharura.

Mganga Mkuu Wilaya ya Makete Ligobert Kalisa amesema kufuatia kufungwa kwa vifaa hivyo zoezi la kutoa huduma linatarajiwa kuanza haraka iwezekanavyo kwa ajili ya kusaidia wagonjwa wanaofika Hospitalini hapo kupata huduma za Afya.

Madaktari na wataalamu mbalimbali wakipata maelezo kuhusu vifaa vilivyofungwa kwenye Jengo la Dharura Hospitali ya Wilaya Makete
Mwonekano wa baadhi ya Vifaa katika Jengo la Dharura Hospitali ya Wilaya Makete