Kitulo FM

UWT Njombe wapanda miti Ilumaki Sekondari

January 29, 2023, 7:54 am

Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Njombe wamefanya Maadhimisho ya miaka 46 ya Chama cha Mapinduzi Wilayani Makete kwa kupanda miti kuzunguka eneo la shule ya Sekondari Ilumaki iliyopo Kata ya Lupalilo Wilaya ya Makete.

Mbaraza Mkoa wa Njombe Anna Mwalongo akipanda mti wa Parachichi shule ya Sekondari Ilumaki

Zoezi hilo limefanywa na wanawake hao wakiongozwa na Katibu wa UWT Mkoa wa Njombe Rehema Zuberi akiwa ameambatana na Mwakilishi wa Mkutano Mkuu Taifa kupitia UWT Mkoa wa Njombe Bi. Anna Mwalongo, amewasihi wananchi kuendelea kupanda na kutunza miti kwa lengo la kulinda Mazingira.

Kwa upande wake Katibu wa UWT Wilaya ya Makete Zubeda Bilali amesema Chama kinatambua mchango mkubwa unaotolewa na Serikali katika sekta ya Mazingira na nyinginezo huku akiwasihi wanafunzi kuitunza miti hiyo kwa manufaa ya sasa na baadaye.

Katibu UWT Wilaya ya Makete Zubeda Bilali akipanda mti wa parachichi

Mkuu wa shule hiyo Mwl. Christoms Mturo akiishukuru Serikali kwa kutoa fedha nyingi kujenga miundombinu ya kujifunzia wanafunzi kwa lengo la kuwa nna kizazi chenye uelewa katika mambo mbalimbali hapo baadaye.

Kwa niaba ya wanafunzi wengine Queen Sanga amepongeza jitihada za Chama na UWT kwa kuamua kufanya zoezi hilo katika shule hiyo huku wakiahidi kuendelea kutunza mazingira ya shule hiyo.