Kitulo FM

Tumieni Vishikwambi kwa manufaa ya Elimu- Mkurugenzi Makete

January 29, 2023, 8:12 am

Mkurugenzi Mtendaji Halashauri ya Wilaya Makete William Makufwe amewataka walimu kutunza Vishikwambi walivyopewa na kuvitumia kwa lengo lililokusudiwa.

Makufwe ametoa rai hiyo wakati wa makabidhiano ya Vishikwambi hivyo yaliyofanyika mwishoni mwa mwezi huu Januari, 2023

eMkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Makete William Makufwe akikabidhi vishikwambi kwa walimu wa Shule ya Sekondari Lupalilo

Ameongeza kuwa kwa yeyote atakayebainika kutumia kishikwambi hicho nje ya utaratibu atachukuliwa hatua za kinidhamu.

Mwl. Lunanilo Kilatu kwa niaba ya walimu wengine Wilayani Makete ameishukuru Serikali kwa kutoa vishikwambi hivyo na kuahidi kuendelea kuboresha utolewaji wa Elimu kwa wanafunzi Wilayani Makete.

Zaidi ya vishikwambi 1,200 vimegawiwa kwa walimu wote shule za Msingi na Sekondari Wilayani Makete Mkoani Njombe