Kitulo FM

Mfuko wa Jimbo Makete waongezeka kutoka Milioni 36 hadi Milioni 59

January 29, 2023, 7:43 am

Mbunge Jimbo la Makete Mhe. Festo Sanga

Serikali imeongeza mfuko wa Jimbo la Makete kutoka Milioni 36,282,000 kwa mwaka 2021/2022 hadi kufikia Milioni 59,647,000 kwa mwaka 2022/2023.

Kupitia Kikao cha Baraza maalumu la Madiwani kilichofanyika leo Tarehe 27 Januari 2023 cha kupitisha Bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024, Kikao hicho kimekubaliana kupokea taarifa ya Mfuko wa Jimbo katika taarifa ya Baraza la Madiwani lijalo mwezi Februali, 2023.