Kitulo FM

Wazazi wawajibike kulea Watoto-Mwanasheria Makete

January 27, 2023, 7:28 am

Wananchi wametakiwa kuhakikisha wanahudumia Familia hususani watoto pale wazazi/wanandoa wanapokuwa wametengana kwa sababu mbalimbali.

Rai hiyo imetolewa na Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Wilaya ya Makete Ndg. Appolo Laizer akizungumza na Kitulo FM kwenye Kipindi cha Daladala tarehe 27 Januari, 2023.

Laizer amesema inatokea wazazi hawaishi pamoja kwa sababu ya kutengana au kuwa mbali wanapaswa kuhakikisha watoto wanalelewa na wazazi wa pande zote mbili bila kujali changamoto za kimaisha.

Laizer ameeleza kuwa Kuelekea maadhimisho ya siku ya Sheria yenye Kauli Mbiu “Umuhimu wa Utatuzi wa Migogoro kwa njia ya Usuluhusishi katika kukuza uchumi endelevu: Wajibu wa Mahakama na Wadau” wananchi wanapaswa kutambua umuhimu wa Malezi bora kwa kutoa huduma zote muhimu kwa watoto wao.