Kitulo FM

Jamii ijikite kusuluhisha Migogoro-Mhe. Ivan Msaki

January 27, 2023, 7:55 am

Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya makete wanne kutoka kushoto akiwa na wakufunzi wa chuo cha sayansi ya afya bulongwa

Hakimu mkazi mfawidhi Mahakama ya Wilaya ya Makete Mh. Ivan Msaki amesema jamii ikijikita katika utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi kutaifanya jamii yenyewe  kuishi bila uhasama.

Mh. Msaki ameyasema hayo januari 25,2023  wakati akizungumza na wanafunzi wa chuo cha Sayansi ya Afya Bulongwa wakati wa zoezi la kutoa  elimu kuhusu maswala mbalimbali ya kisheria, katika wiki hii ya kisheria nchini ambayo maadhimisho yake ni  tarehe 1 Februari 2023.

Msaki amesema kama ilivyo kauli mbiu ya wiki ya kisheria nchini isemayo Umuhimu wa utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuruhishi katika kukuza uchumi endelevu  wajibu wa mahakama na wadau,

Hivyo jamii  kama mlengwa mkuu inapaswa kujikita katika utambuzi wa suala hilo na kulitekeleza

Wanafunzi wa chuo cha Sayansi ya Afya Bulongwa waliopata wasaa wa kuhudhulia darasa la elimu hiyo ya maswala mabalimbali ya kisheria mbali na kupongeza elimu hiyo waitaka mahakama kulifanya ambo la elimu kuhusu maswala ya kisheria kuwa endelevu ili jamii iwe na uelewa mpana kuhusu sheria mbalimbali.

Maadhimisho ya siku ya sheria nchini yalianza tarehe 22/1/2023 na yatahitimishwa tarehe 1/2/2023 katika viwanja vya mahakama ya wilaya ya makete kuanzia saa 2:00  asubuhi.