Kitulo FM

Ujenzi wa Jengo la Halmashauri Makete waanza

January 25, 2023, 12:34 pm

Halmashauri ya Wilaya Makete imeanza Ujenzi wa Jengo (Ghorofa moja) ambalo mpaka kukamilika kwake itagharimu Bilioni 3 ikiwa mpaka sasa kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali imetofedha Bilioni 1 kuanza ujenzi

Akieleza kuhusu mradi huo Mtaalamu kutoka Divisheni ya Ujenzi White Edward amesema Ujenzi huo unafanyika kupitia Chuo cha Sayansi na Teknolojia Must Mbeya kupitia kamouni yake ya MCB Company Limited

Kamati ya Siasa CCM Wilaya ya Makete imefika eneo linapojengwa jengo hilo (Ngiu) kwa lengo la kuangalia mwanzo wa ujenzi na kuhimiza umakini katika usimamizi

Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mhe. Hawa Kader amesisitiza uwazi katika manunuzi ambayo yanafanywa na Halmashauri

Mwenyekiti wa CCM Wilaya Ndg. Clement Ngajilo amepongeza Viongozi wa Halmashauri kwa ubunifu katika kipindi kifupi huku akimshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. @samia_suluhu_hassan kwa kutoa fedha za ujenzi huo.

Diwani Kata ya Iwawa Mhe. Francis Chaula kwa niaba ya wananchi wa mji mdogo Iwawa ameishukuru Serikali kwa kutekeleza miradi mikubwa katika Kata yake ikiwemo Ujenzi wa Hospitali na Jengo la Halmashauri