Kitulo FM

MNEC Njombe ampongeza DC Makete kuaminiwa na Rais

January 25, 2023, 4:00 pm

Mwakilishi wa Mkutano Mkuu CCM Taifa Mkoa wa Njombe (MNEC) Ndg. Abraham Okoka amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Makete Mhe. Juma Sweda kwa kuaminiwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuendelea kuwatumikia wananchi wa Makete

MNEC ametoa pongezi hizo leo akiwa kwenye Mkutano wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya uliofanyika ukumbu wa Francis Chaula Makete mjini

Amesema kazi kubwa inayofanywa na Mkuu huyo wa Wilaya ya kuchochea maendeleo na kusikiliza changamoto zinazowakabili wananchi kila kijiji imekifanya Chama kuamini utenda kazi wake huku Rais Samia Suluhu Hassan akiamini uwepo wake katika Wilaya ya Makete utaifanya Makete kuendelea kubadilika kwa kasi.

Rais wa Tanzania Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya wapya 37, kuwahamisha vituo vya kazi wakuu wa Wilaya 48 na wengine 55 kubakia kwenye Vituo vyao vya kazi akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Makete