Kitulo FM

Hatuwezi kuwa na Furaha wakati watu wetu wanateseka-Mhe. Sweda

January 25, 2023, 2:13 pm

Mkuu wa Wilaya ya Makete Mhe. Juma Sweda amesema Halmashauri na TARURA inapaswa kuhakikisha wannanchi waa Kigulu wanapata huduma ya Barabara kulingana na kukosa huduma hiyo kwa miaka mingi kwa kuwa hali si nzuri.

Mhe. Sweda amesema Mwanamke akipatwa na uchungu saa 8 usiku nna hawezi kujifungua kawaida kuna uwezekano mkubwa wa kupoteza uhai kwa kukosa huduma ya usafiri.

Amewataka TARURA kuhakikisha wanarekebisha barabara kwa muda mfupi kwa kuwa fedha wanayo walishapata kutoka Serikalini hivyo wawajibike haraka kunusuru wananchi wa Kigulu.