Kitulo FM

Zaidi ya Milioni 100 kujenga Bweni Usililo Sekondari

January 24, 2023, 6:42 am

Serikali imetoa fedha zaidi ya Milioni 103 kupitia mfuko wa kusaidia Kaya Maskini TASAF kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wavulana wanaosoma shule ya Sekondari Usililo iliyopo Kata ya Luwumbu huku fedha inayobaki ikiwa ni nguvu kazi ya Wananchi ambayo ni kuandaa uwanja, Kusogeza mawe na kuandaa tofali

Kamati ya Siasa CCM Wilaya ya Makete imetembelea mradi huo leo na kuwasihi wananchi wa Kata ya Luwumbu kuongeza nguvu kazi ya mawe ili kukamilisha mradi huo kama ilivyopangwa ili wanafunzi waanze kulitumia bweni hilo.

Mradi huo ulianza kutekelezwa mwezi wa 4, 2022