Kitulo FM

Walima barabara kwa Majembe kunusuru hali mbaya ya Usafiri

January 24, 2023, 6:33 am

Wananchi wa Kijiji cha Unyangala wakilima barabara kwa majembe na chepe ili kuondoa kifusi kilichoziba barabara hiyo eneo la Utengule baada ya kukosa huduma ya mawasiliano tangu kipindi cha Masika mwaka uliopita.

Barabara hiyo ilijifunga baada ya udongo kuporomoka na kuziba kabisa barabara na kuwafanya wananchi kukosa mawasiliano

Zoezi la kuondoa udongo katikati ya barabara hiyo limeanza tangu Alhamisi wiki iliyopita na wananchi wameendelea tena jumatatu ya tarehe 23 Januari 2023 kwa wananchi kufika eneo hilo na kuondoa udongo ili kupata mawasiliano yaa usafiri angalau hata wa pikipiki maarufu kama bodaboda

Kwa mujibu wa wananchi wa kijiji cha Unyangala na Utengule eneo hilo inaelezwa kuwa kulingana na kuwa na milima kwa zaisi ya 90% ya vijiji hivyo vilivyo katika milima ya Livingstone.

Wananchi wa kijiji hicho kwa nyakati tofauti wameiomb Serikali kuangalia namna ya kuhamisha barabara hiyo kwa kuwa ilipopita sasa ni eneo hatari kwa wananchi kwa kuwa hii si mara ya kwanza kuporomoka kwa barabara katika eneo hilohilo