Kitulo FM

Ukaguzi wa Ujenzi Kituo cha Afya Bulongwa

January 24, 2023, 6:36 am

Kamati ya Siasa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Makete ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Clement Ngajilo wamefika kukagua ujenzi wa Kituo cha Afya Bulongwa wenye thamani ya Milioni 500 na kupongeza jitihada za Serikali na wananchi katika ujenzi huo

Fedha hizo zimetolewa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza Serikali ilitoa Milioni 250 na awamu ya pili Milioni 250

Mpaka sasa ujenzi wa Kituo hicho umefikia hatua za mwisho huku Kamati hiyo ikishauri mafundi kuongeza kasi ili kukamilisha na wananchi waanze kupata huduma za Afya