Kitulo FM

Elimu itolewe utunzaji wa Mazingira Makambako-Njombe

January 18, 2023, 10:39 am

 

Halmashauri ya mji wa Makambako imetakiwa kutoa elimu kuhusiana na usafi wa mazingira ili kuhakikisha maeneo yote yanafanyiwa usafi lengo likiwa ni kukabiliana na magonjwa ambukizi.

Wakizungumza na Kituo hiki baadhi ya wananchi wa mtaa wa rajabu mahakamani uliopo kata ya kitisi mjini Makambako,Evaristo Mgeni,Teodola Komba na Hawadi Nganelavanu wamesema yapo baadhi ya maeneo yameachwa yakiwa machafu hasa katika kipindi hiki cha mvua hali ambayo inaweza kuchochea magonjwa ambaukizi.

Wananchi hao wamesema ili kukabiliana na hali hiyo ni lazima halmashauri kupitia serikali za mitaa iweke utaratibu wa kufanya usafi katika maeneo hayo.

Akizungumzia kuhusiana na changamoto hiyo mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Rajabu Mahakamani David Msakala amekiri kuwepo kwa uchafu katika maeneo hayo hasa kwenye mitalo ya kupitishia maji taka na kueleza kuwa atahakikisha usafi unafanyika.

Naye Afisa Mtendaji kata ya kitisi Daria Kilasi amesema licha ya uchafu bado kumekua na changamoto ya wananchi kulima na kupamba mazao marefu katikati ya mji jambo ambalo ni kinyume na taratibu na kueleza kuwa kupitia viongozi wa mitaa watahakikisha sheria inafuata mkondo wake.